} });
 

 

ALIYEKUWA mshambuliaji nyota wa vilabu vya AC Milan, Real Madrid na timu ya taifa ya Brazil Robinho, amehukumiwa kufungwa miaka tisa jela na mahakama ya rufaa ya nchini Italia, baada ya kukutwa na kosa la ubakaji wa binti mdogo alilolifanya miaka saba iliyopoita nchini humo.

 

Robinho na rafiki yake Ricardo Falco wameripotiwa kumbaka binti huyo raia wa Albania aiishie nchini Italia kwenye ukumbi wa starehe wakati binti huyo akiwa anasheherekea kumbukizi ya siku yake ya kuzaliwa kwa kutimiza miaka 23 mwaka 2013.

 

Wakili wa binti huyo, Jaccopo Gnochi, amesema ”hukumu hiyo ni mfano kwa wengine juu ya kulinda utu wa mwanake na kuonyesha ni jinsi gani mfumo wa sheria unavyofanya kazi”.

 

Robinho anakumbukwa na wafuatiliaji wengi wa soka ulimwenguni kwa kuwa na uwezo wake mkubwa wa kuuchezea mpira, kuwatoka walinzi kwa chenga kali na kufunga mabao ya kuvutia akiwa na vilabu vya AC Milan, Real Madrid, Man city na timu ya taifa ya Brazil miaka ya 2008-13.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top