} });
 

 

Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dk. Faustine Ndugulile ametoa miezi mitatu kwa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kumaliza changamoto za bando na vifurushi zinazotolewa na kampuni za simu za mkononi kwa wananchi.

Dk. Ndugulile ameyasema hayo Desemba 28, alipotembelea TCRA ikiwa ni moja ya taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo kwa lengo la kufahamiana, kutambua majukumu yao na kuzungumza na Bodi, Menejimenti na wafanyakazi wa taasisi hiyo ili kuwa na uelewa wapamoja na kushirikiana kwa kufanya kazi kwa pamoja katika kuhudumia wananchi kuelekea Mapinduzi ya Nne ya Viwanda na kuiwezesha Tanzania kuwa na uchumi wa kidijitali.

Amesema, ni lazima TCRA ishughulikie malalamiko ya wananchi kwa kuwa wananchi hawana imani na vifurushi na bando, na kuwe na mfumo wa kuhakiki gharama halisi za mawasiliano kuendana na fedha aliyotoa mwananchi na kuwe na namba ya bure ambayo wananchi watapiga ili kuwasilisha malalamiko yao ili kuwawezesha wananchi kuongeza imani yao kwa serikali.

“Ni heri tufanye maamuzi mabaya kuliko kutokufanya maamuzi, nataka mshirikiane na Baraza la Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano (TCRA – CCC) kumaliza changamoto hii kwa kuwa Watanzania sio wajinga, nataka aone kapata shilingi moja anaitumia shilingi moja yake kupiga simu,”  Dk. Ndugulile.

Pia, amewataka kuhakikisha kuwa, chaneli tano za bure za runinga inaonekana hata baada ya muda wa kulipia kumalizika kwa kuwa chaneli hizo hazionekani kwenye baadhi ya ving’amuzi.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top