} });
 

 

BAADA ya kusambaa kwa taarifa mitandaoni zinazodai kwamba aliyekuwa mgombea urais wa chama cha ACT-Wazalendo, Bernard Membe, kuwa atajitoa katika chama hicho Januari Mosi, mwakani, uongozi wa chama hicho umesema haupo tayari kuzungumzia suala hilo kwa sasa.

 

Katibu Mkuu wa chama hicho, Ado Shaibu, amesema hawapo tayari kuzungumzia suala hilo kwani kwa sasa wana mambo ya kuwaelekeza Watanzania baada ya kikao cha Kamati Kuu kumalizika jana Desemba 5, 2020.

 

“Watanzania wanahitaji kufahamu Kamati Kuu imeamua nini kuhusu masuala yaliyopo mbele yetu ambayo tulijadili na tutatoa taarifa hapo baadaye na siyo masuala ya Bernard Membe, siyo muda wake kwa sasa, nitafutwe wakati mwingine,” amesema.

 

Membe aliyewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Nje ni mwanachama mwenye kadi namba 2 na Mshauri Mkuu wa chama hicho ambaye alijiunga na ACT- Wazalendo Julai 16, 2020, na aligombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama hicho akaibuka na kura 81,129 sawa na asilimia 0.5% ya kura zote.

 

Membe kada wa muda mrefu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) alijiunga chama cha ACT-Wazalendo  baada ya Februari 28, 2020 kufukuzwa uanachama wa CCM na Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya chama hicho.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top