
MUUNGANO wa vyama vya kisiasa wa FCC wa aliyekuwa rais wa Congo (DR), Joseph Kabila, umekiri kuwa kung’olewa kwa, Jeanine Mabunda kwenye wadhifa wa Spika wa Bunge la nchi hiyo ni vita kubwa.
Muungano wa FCC ulioanzishwa na Kabila umetoa wito kwa wafuasi wa muungano huo kufunga vibwebwe, wakati wengi wanaendelea kujiuliza maswali kadhaa kuhusu hatma ya FCC.
Baada ya Spika huyo kutimuliwa mamlakani na kuvunjwa kwa ofisi ya Bunge (kuondolewa kwa wajumbe watano kati ya sita wa kamati kuu ya Bunge), PPRD, chama cha Kabila, hatimaye kimekiri kushindwa.
“Ushindi hauji kila wakati. Wacha tu tufikirie haraka jinsi ya kuimarisha muungano wetu. Maumivu ni makubwa, lakini tusikate tamaa. Wacha tuendelee na vita hivi, wanaharakati wapendwa,” alisema
Patrick Nkanga, mmoja wa makada wa PPRD, amebainisha kuwa wakati umewadia wa kufanya mabadiliko makubwa kwa PPRD na pia kwa FCC.
Post a Comment