} });
 

 

Jeshi la polisi Wilaya ya Igunga mkoani Tabora limefanikiwa kumkamata kigogo mmoja ambaye ni wakala maarufu wa mabasi, Hamisi Masoud (37) mkazi wa mtaa wa Mwayunge Kata ya Igunga mjini na kumfikisha katika mahakama ya wilayani hapa kwa tuhuma za kubaka na kulawiti mwanamke wa miaka (31).

 

Awali mwendesha mashitaka wa polisi Wilaya ya Igunga, Elimajid Kweyamba aliiambia mahakama mbele ya hakimu wa wilaya hiyo, Lydia Ilunda kuwa mshitakiwa Hamisi Masoud anashitakiwa kwa makosa mawili.

 

Kweyamba alisema kosa la kwanza anatuhumiwa kulawiti na alitenda kosa hilo kinyume na kifungu 154 (1) (a) kanuni ya adhabu sura ya 16 mapitio ya 2019 inayozuia kutenda makosa kama hayo.

 

Alisema Novemba 30/2020 majira ya kati ya saa mbili usiku hadi saa sita usiku katika mtaa wa Mwayunge Kata ya Igunga mjini, mshitakiwa Hamisi Masoud anadaiwa alifanya mapenzi na mwanamke wa miaka 31 ambaye jina limehifadhiwa mkazi wa mtaa wa Mwayunge kinyume na maumbile.

 

Aidha Majid alisema shitaka la pili ni linalomkabili mshitakiwa ni kudaiwa kubaka kinyume na kifungu 130(1)(2)(b) na 131 kanuni ya adhabu sura ya 16 mapitio ya 2019 inayozuia kutenda makosa kama hayo.

 

Alisema katika tarehe hiyo na muda huo mshitakiwa Hamisi Masoud kwa makusudi kwa kutumia nguvu na vitisho anadaiwa alifanya mapenzi na mwanamke huyo bila hiyari yake mwanamke.

 

Baada ya kusomewa mashitaka hayo mawili mshitakiwa Hamisi Masoud alikana kutenda makosa hayo ambapo kesi hiyo imeahirishwa hadi Desemba 18/2020 itakapoanza kusikilizwa kwa awali na mshitakiwa amepelekwa mahabusu baada ya kushindwa kutimizwa masharti ya dhamana.

 

Ili adhaminiwe mahakama ilimtaka kuwa na wadhamini wawili huku kila mmoja akitakiwa awe na mali isiyohamishika yenye thamani ya shilingi milioni 6.

 

Hata hivyo mwendesha mashitaka alisema bado mtuhumiwa anaandaliwa shitaka la tatu la shambulio analodaiwa kulifanya kwa mwanamke huyo.

 

Mganga Mkuu wa Wilaya ya Igunga Dk. Deus Ruta alithibitisha kumpokea mama huyo Desemba 1/2020 na kumfanyia uchunguzi na kuonyesha aliingiliwa sehemu zake zote za siri na alipigwa, walimpatia matibabu kisha kumruhusu.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top