} });
 

 

MAJIMBO manne nchini Nigeria yametoa amri ya shule kufungwa baada ya wanafunzi zaidi ya 100 kutekwa katika jimbo la Katsina.  Shule hizo zimefungwa katika majimbo ya Kano, Kaduna, Zamfara na la Jigawa.

 

Chama cha walimu nchini Nigeria kimetishia kufanya mgomo kuhusiana na kuzorota kwa usalama nchini humo kikisema wanafunzi na walimu ndiyo wamelengwa zaidi na  watekaji, wapiganaji hao.

 

Wiki iliyopita mamia ya wanafunzi walitekwa katika shule moja ya sekondari ya serikali inayofundisha masomo ya sayansi katika jimbo la Kankara ambapo wanamgambo wa Kiislamu wa kundi la Boko Haram walikiri kufanya shambulio hilo.

 

Serikali ya shirikisho bado haijaeleza imefikia hatua gani katika juhudi za kuwaokoa wanafunzi 333  ambao wamepotea mpaka sasa.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top