} });
 


Leo Jumatano, Desemba 9, Namungo FC ina kazi ya kusaka pointi tatu mbele ya Biashara United, Uwanja wa Majaliwa saa 10:00. Simba pia itakuwa na kibarua cha kusaka pointi tatu mbele ya Polisi Tanzania, saa 1:00 usiku Uwanja wa Mkapa.

 

Mechi zote za leo ni viporo kwa sababu timu ya Namungo ilikuwa na kazi ya kuwakilisha nchi mwenye mchezo wa kimataifa dhidi ya Al Rabita ya Sudan Kusini ambapo mchezo wa awali Namungo ilishinda mabao 3-0 Uwanja wa Azam Complex.

 

Inasonga mbele baada ya Shirikisho la Soka Afrika, (Caf) kuufuta mchezo wa marudio uliotarajiwa kuchezwa Desemba 6 Uwanja wa Azam Complex kutokana na wapinzani hao kushindwa kukidhi vigezo kuhusu waamuzi.

 

Kwa upande wa Simba wao walikuwa na kibarua mbele ya Plateau United, mchezo wa awali ilishinda bao 1-0 ugenini lililofungwa na Clatous Chama na mchezo wa marudio walilinda ushindi wao hivyo wanasonga hatua ya pili na kukutana na FC Platinum ya Zimbabwe.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top