} });
 


Supastaa wa Bongo Fleva, Omary Nyembo ‘Ommy Dimpoz’, amefichua siri juu ya kufuru zake za pesa. Dimpoz amekuwa akila bata za hatari kwenye viwanja vikubwa vya bata duniani huku akiishi maisha ya ‘peponi’ na kuendesha ndinga za kifahari, kiasi cha kuwatoa udenda vijana wenzake.

 

Pamoja na bata hizo za bei mbaya, lakini Dimpoz amekuwa hategemei kufanya shoo au kuuza muziki wake kwenye mitandao kama wanavyofanya wasanii wengine Bongo.

 

Katika mahojiano maalum (exclusive interview) na Gazeti la IJUMAA, Dimpoz anafunguka juu ya watu wanaomchukulia poa na kumuona wa kawaida bila kujua kwamba, ana pesa, ila huwa hapendi matangazo au kujionesha.

 

Dimpoz ambaye kwa sasa amekula shavu la kuwa mmoja wa majaji kwenye Shindano la Bongo Star Search (BSS) 2020 anasema kuwa, watu waache kuwaona watu kama wasiokuwa na chochote kwa sababu siyo lazima kujionesha pale unapokuwa na kitu (pesa).

 

“Kuna kitu watu wengi hawakijui tu na wanaweza kuzungumza chochote, lakini ukweli ni kwamba mimi ninafanya kazi zangu vizuri sana, ninapiga madili yangu ipasavyo hivyo watu wasione watu hawajichanganyi, wakaona kama hawana chochote cha kujikimu kwenye maisha yao ya kila siku,” anasema Dimpoz.

 

Dimpoz anasisitiza kuwa, anamshukuru Mwenyezi Mungu kwa kumpa madili mengi kwani anafanya kazi na makampuni mengi kama GSM na analipwa vizuri, lakini hapendi kujionesha kwa sababu hakuna ambaye atamsaidia hata kama akijionesha.

 

“Ni kweli maisha mazuri ninayo, lakini siwezi kuyaweka mitandaoni maana huko sioni nitakuwa ninamuonesha nani kwa sababu hata kama sasa hivi nitakuwa sina, niliowaonesha hawawezi kunisaidia chochote,” anasema Dimpoz ambaye alipitia wakati mgumu mno alipopata tatizo la kiafya na kufanyiwa upasuaji wa koo.

 

Dimpoz anafunga mwaka 2020 baada ya hivi karibuni kusaini mkataba na kampuni ya muziki ya Sony Music Entertainment Africa ya jijini Johannesburg nchini Afrika Kusini. Mkataba huo mpya unamfanya Dimpoz kujivunia kuwa ni msanii wa kiwango cha juu barani Afrika.

 

Dimpoz amesema kuwa, anafurahia kulamba dili hilo nono ambapo ameashaanza kuachia kazi kama Wimbo wa Dede kutoka kwenye album yake ijayo. Wimbo huo mpya kutoka kwa Dimpoz amewashirikisha DJ Tira, Dladla Mshunqisi na Prince Bulo.

 

“Ni hatua muhimu sana kwenye muziki wangu na ni wakati sahihi kwenye maisha yangu,” anasema Dimpoz. Dimpoz alianza muziki kama mwimbaji wa bendi ya msanii wa Bongo Fleva, Khaleed Mohamed ‘TID’ iitwayo Top Band kabla ya baadaye kuibuka kama mwanamuziki wa kujitegemea na wimbo wake wa kwanza ulikuwa ni Nai Nai akimshirikisha mfalme wa muziki huo, Ali Saleh Kiba ‘King Kiba’ hivyo TID ni kama alimfungulia milango ya muziki, kwani baadaye alitoka na Wimbo wa Mama akiwa ameshirikiana na msanii mkali wa Dansi Bongo, Christian Bella.

 

Me and You ni wimbo alioshirikiana na msanii Vanessa Mdee ukamtambulisha ndani ya mipaka ya Afrika Mashariki na hapo ndipo Dimpoz alipoendelea kuwasha moto kwenye ulimwengu wa muziki. Nyimbo zake nyingine kali ni Hello Baby aliomshirikisha msanii Avril kutoka Kenya, Achia Body, Tupogo, Wanjera, Ndagushima na Kajiandae.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top