} });
 

 

SVEN Vandenbroeck, Kocha Mkuu wa Simba, amewataka wachezaji wake kucheza kwa tahadhari katika kusaka matokeo ndani ya uwanja kwani wana kibarua cha kukusanya pointi tatu kwenye kila mechi za Ligi Kuu Bara.

 

Raia huyo wa Ubelgiji, amesema kuwa, wanapaswa kucheza kwa umakini kusaka matokeo huku wakichukua tahadhari kwa sababu ya mechi zingine zilizo mbele yao.

 

“Baada ya mechi dhidi ya Plateau United, katikati ya wiki tutakuwa na mechi kule Mbeya, sasa hapo kwa namna yoyote ni lazima wachezaji wacheze kwa tahadhari.

 

“Lengo kwenye mechi zetu za ligi ni kuendeleza kasi ile ambayo tuliishia kwenye mchezo wa mwisho ili kupunguza pointi ambazo tumezidiwa na wapinzani wetu.

 

“Tunatambua kwamba tuna kazi ya kutetea ubingwa, hilo halitawezekana ikiwa tutashindwa kupata ushindi,” alisema Sven. Katika msimamo wa Ligi Kuu Bara, Simba ipo nafasi ya tatu ikiwa na pointi 23 baada ya kucheza mechi 11. Yanga inaongoza ligi ikikusanya pointi 31 baada ya kucheza mechi 13.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top