![]() |
Naibu Waziri wa Kilimo Hussein Bashe akitoa maagizo kuhusu ukarabatiwa miundombinu ya umwagiliaji Wilayani Bahi. |
Naibu Waziri wa Kilimo Hussein Bashe amesema tafiti za kilimo cha ngano katika mikoa ya Dodoma, Mbeya na Arusha zilizofanyika hivi karibuni zimetoa matokeo chanya ambapo aina tatu za mbegu za ngano zilizofanyiwa majaribio zimeonyesha uwezo mkubwa wa kustawi nakutoa mavuno ya kuridhisha katika mikoa hiyo.
Akizungumza wakati wa ziara ya kikazi wilayani Bahi , Naibu Waziri Bashe amezitaka taasisi za Utafiti wa kilimo (TARI), Taasisi ya Mbegu (ASA), Tume ya Taifa ya Umwagiliaji(NIRC) pamoja na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Mazao nchini (DCD) kushirikiana katika kutekeleza mpango wakilimo hicho ili kupata matokeo chanya.
“Hatua hiyo inakwenda sambamba na sera ya Maendeleo ya Taifa ya mwaka 20 - 25 inayoelekeza taifa kuzalisha zao la ngano kwawingi ili kusitisha uagizaji wa bidhaa hiyo nje ya nchini.” Alisisistiza
Naibu Waziri Bashe alimaliza kwa kusema kuwa, kwa kuanzia zoezi hilo litatekelezwa katika Skimu kumi na nne Wilayani Bahi.
Facebook Blogger Plugin by TeachMaker
Post a Comment