} });
 

 

Taharuki na mshangao wa aina yake umetokea kwa wakazi wa Mbagala Kwa Mbiku, jijini Dar es Salaam, baada ya mtoto wa Darasa la Pili (Shule na jina lake linahifadhiwa) kupewa ujauzito na njemba mweny umri wa miaka 37.

 

Njemba huyo anayetuhumiwa kumbaka mtoto huyo ametajwa kwa jina la Frank Ngede na kwamba baada ya kushtukia kuwa polisi wanamsaka kwa tuhuma za ubakaji, ametoroka.

 

Akizungumza kwa masikitiko mwishoni mwa wiki iliyopita na mwandishi wetu mama wa mtoto huyo Amina Awadh alisema kitendo alichofanyiwa mwanaye kimemuumiza.

“Nimekuwa nafuatilia afya ya mwanangu kwa ukaribu, mwezi wa 11 nikaona mabadiliko.

 

“Nikamuuliza lakini hakunijibu, akawa anaendelea kwenda shule kama kawaida.

“Siku moja akanifuata akaniambia ‘mama naumwa’, tarehe tano mwezi wa 12, 2020 usiku nikamchukua kumpeleka hospitali.

 

“Baada ya kufika, daktari akamchukua vipimo na mwisho wa siku majibu yakatoka kuwa binti yangu ni mjamzito.


“Nilishtuka sana, basi tukarudi nyumbani ndipo nilipoanza kumuuliza hii mimba ni ya nani akaniambia ni ya baba fl’ani, (akamtaja mhusika) na kunisimulia tukio zima jinsi lilivyokuwa.

 

“Kwa kweli nilipatwa na hasira sana nikajikuta nakalia kwa muda mrefu, sasa wakati nalia aliyembaka mwanangu na mkewe wakaja ndani (ni majirani kwa mujibu wa maelezo) ili kujua nalilia nini.


“Walipofika sikuwaambia chochote sasa nahisi walivyotoka ndio mwanaume alikuwa ameshajua kuwa nina fahamu kila kitu ndio hapo alipochukua uamuzi wa kutoroka.

 

“Nilienda kituo cha Polisi Mbagala Maturubai wakanipa PF3 nikaenda kumpima mtoto upya katika Hospitali ya Temeke na huko majibu yalitoka hivyohivyo kuwa ni mjamzito wa miezi miwili na nusu.


“Kama mzazi naumia sana, mwanangu bado mdogo na anahitaji kutimiza malengo yake, naomba hatua za kisheria zichukue mkondo wake, aliyembaka katoroka na hatujui ametorokea wapi,” alisema Amina kwa uchungu.

 

MKE WA ALIYEBAKA AANGUA KILIO

Kama ilivyokuwa taharuki kwa watu wengine mke wa mtuhumiwa aitwaye Winfrida James naye alijikuta katika wakati mgumu na kujikuta akimwaga machozi baada ya kuambiwa kuwa mumewe amebaka mtoto wa miaka 13 ambaye ametajwa kuwa alichelewa kuanza shule ndiyo maana yuko darasa la pili.

 

Mwandishi wetu alipomuuliza Winfrida amepokea taarifa za mumewe aliyebahatika kuzaa naye watoto watatu kuhusishwa na tukio la ubakaji alisema:


“Sisi hapa ni wapangaji, nakumbuka hiyo siku mama (jina linafichwa) analia watu walijaa nyumbani kwake, nilipouliza kuna nini hakunipa jibu.

 

“Basi kesho yake jumatatu mume wangu akaniaga kuwa anaenda kazini, lakini cha kushangaza hiyo siku hakurudi nyumbani mpaka leo.


“Baadaye ndiyo askari wakaja kumuulizia na kuniambia kuwa mume wangu anakosa ya ubakaji, niliumia sana, sijui ametorokea wapi, kaniachia watoto watatu na mmoja ana mwezi mmoja sina hata pesa ya kula na hapa kodi ya nyumba imeisha nimepewa hifadhi tu na kanisa,” alisema Winfrida.

 

MCHUNGAJI NAYE AONGEA

UWAZI lilizungumza na mchungaji wa kanisa la Shekina lililopo Mbagala, Sadoki Barugizi ambaye ndiye baba wa kiroho wa mtuhumiwa pamoja na mkewe ili kujua amepokea taarifa ya muumini wake kuhusishwa na ubakaji ambapo alisema:

 

“Nilipokea hii taarifa siku ya Jumatatu (wiki iliyopita), nilikuwa Mkuranga (mkoani Pwani) kuwa kuna tukio limetokea eneo ambalo mimi nafanyia huduma.


“Baada ya kupata taarifa hizo nilisikitika sana kwa sababu hawa ni watu ambao nawafahamu na wanaabudu kanisani kwangu, hivyo kama ni kweli hilo tukio limefanyika basi tunaomba sheria ifuate mkondo wake,” alisema Barugizi.

 

MSIKIE MTOTO MWENYEWE

Akizungumza na UWAZI kwa uchungu mtoto aliyebakwa na kupewa ujauzito alisimulia namna ambayo amekuwa akifanyiwa ukatili huo wa kingono na mtuhumiwa hadi kupewa ujauzito, alisema:


“Nakumbuka ilikuwa saa mbili usiku nilikuwa nipo bafuni naoga, mara nikashangaa mtu ameingia, ghafla akaniambia usipige kelele ndiyo akaanza kunifanyia hicho kitendo.

 

“Akaniambia nikijaribu kusema kwa mtu atanichoma kisu, kwa kuwa nilikuwa naogopa ikabidi nikae kimya, nakumbuka alinipa shilingi 1000.


“Baada ya hapo nikarudi ndani nikalala, siku nyingine akanifuata tena ila safari hii akanipeleka kwenye jumba bovu basi ndiyo ikawa tabia yake mpaka nilipojikuta mjamzito,” alisema mtoto huyo mbele ya mama yake huku akimwaga machozi.

 

Uwazi lilifanya jitihada za kuwatafuta viongozi wa serikali ya mtaa ili wazungumzie hili lakini kwa bahati mbaya mwandishi wetu hakufanikiwa kuwapata.

Uwazi linalaani ukatili wa kingono dhidi ya mtoto huyo na linaomba mhalifu asakwe popote alipo ili sheria ichukue mkondo wake.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top