} });
 


Mchezaji wa zamani wa Man United Patrice Evra amefunguka kuwa Mchezaji mwenzake wa Ufaransa na legend wa Arsenal Thierry Henry aliwahi kumualika nyumbani kwake waangalie nae game ya Arsenal lakini alizima TV mara tu baada ya kuona Granit Xhaka kapewa kitambaa cha unahodha.

“Thierry Henry alinialika nyumbani kwake tuangalie game ya Arsenal, nilienda ila Thierry Henry ghafla alizima TV na kuniambia samahani siwezi kuangalia Xhaka anakuwa nahodha wa klabu yangu” Patrice Evra

Kauli hiyo ya Evra inakuja muda mfupi baada ya Arsenal kupoteza mchezo kwa kupigwa 1-0 vs Burnley huku Xhaka akiishia kuoneshwa kadi nyekundu dakika ya 56.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top