} });
 


Mpwa wa Rais Donald Trump wa Marekani amesema, Rais huyo ni mhalifu, katili na haini na kwamba jela ndipo mahali anapostahili kupelekwa baada ya kuondoka Ikulu.

Akihojiwa na Shirika la Habari la Associated Press, mpwa huyo Mary Trump amesema baada ya kuondoka Ikulu Rais Donald Trump inapasa afuatiliwe kisheria na kushtakiwa, ili Marekani isije ikashuhudia kuingia madarakani kwa Rais mbaya zaidi kuliko Trump.

Kuhusu msimamo wa Trump wa kutokubali kwamba ameshindwa katika uchaguzi wa Rais na madai anayotoa kuhusu uchaguzi huo, Mary Trump amesema, mwenendo alioonesha Rais Trump baada ya uchaguzi, unaendana na tabia yake kwa sababu hajawahi kushinda kisheria hata mara moja.

Uchaguzi wa Rais wa Marekani ulifanyika tarehe 3 ya mwezi uliopita wa Novemba na Joe Biden, mgombea urais kwa tiketi ya chama cha Democratic ametangazwa mshindi na kuwa rais mteule wa nchi hiyo.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top