} });
 

 

RAIS  wa Jamhuri ya Demokrasia ya Congo (DRC), FĂ©lix Tshisekedi, aweka wazi mpango wake wa kuvunja Serikali ya Muungano ambayo ina wafuasi wengi wa aliyekuwa rais wa nchi hiyo, Joseph Kabila.

 

Katika hotuba yake,  Tshisekedi amesema, atachagua maofisa wapya na kuunda baraza jipya kwa kuwa bunge la sasa lina wafuasi wengi wa Kabila, huku akisisitiza kuwa kuna ulazima wa kuvunja bunge hilo.

 

Rais huyo aliingia madarakani takribani miaka miwili iliyopita ikiwa ni matokeo ya makubaliano kati yake na Kabila kufuatia uchaguzi ambao  walidai ulikuwa na udanganyifu.

 

Hivi karibuni, Umoja wa Mataifa (UN) na Umoja wa Afrika (AU) umeeleza wasiwasi wake kuhusu mvutano wa kisiasa baina ya pande hizo mbili.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top