} });
 

 

Mratibu wa Kifua Kikuu na Ukoma kutoka Hospitali ya Wilaya ya Tunduru Mkoani Ruvuma, Dkt.Mkasange Kihongole amewaasa wananchi kuacha tabia ya kunywa maziwa ya Ng'ombe yasiyochemshwa na kwamba yanaweza kuwa hatari kwa maambukizi ya ugonjwa wa Kifua Kikuu.

Akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Likweso, Wilaya ni Tunduru, mratibu huyo wa Kifua Kikuu na Ukoma Tunduru Dkt.Mkasange mbali na kutaja maziwa ya ng'ombe yasiyochemswa ni hatari kwa maambukizi ya Kifua Kikuu lakini pia ulaji wa nyama za ndege zisizopikwa vizuri.

Hata hivyo baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Likweso Wilayani Tunduru kilichopo mpakani mwa Tanzania na Msumbiji, wameiomba serikali kudhibiti mlundikano wa wanyama wakiwemo Ng'ombe ambao wanazidi kuongezeka katika maeneo yao wanayoishi.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top