} });
 

 

Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa TAKUKURU Mkoani Kagera inawashikilia Wanafunzi 59, Wakufunzi 4 na Wakuu wa Vyuo wawili kwa tuhuma ya kuhusika katika udanganyifu wa mtihani ulioanza tarehe 7/12/2020.

Mkuu wa TAKUKURU Mkoani Kagera John Joseph ameeleza kuwa watuhumiwa hao ni kutoka Vyuo viwili tofauti ambavyo ni VETA Kagera kilichopo Manispaa ya Bukoba na Chuo cha Tuinuane VTC kilichopo Halmashauri ya Wilaya Bukoba ambapo inadaiwa Wakufunzi kwa kushirikiana na wanafunzi walitengeneza magroup ya WhatsApp ili iwe rahisi kuwapatia majibu.

Sambamba na wao kukamatwa TAKUKURU imekamata simu 66 ambazo inadaiwa zimehusika katika udanganyifu huo, uchunguzi unaendelea na utakapokamilika watafikishwa Mahakamani.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top