} });
 

 

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Dorothy Gwajima amewataka Wakurugenzi na watumishi wa Wizara ya Afya kushirikiana ili kuweza kufikia lengo la kuboresha huduma za afya nchini.

“Mlimpa kibali Rais Magufuli akasimama kifua mbele, kwa wananchi na wakampa ridhaa nyingine tena ya kuongoza Serikali hii, kuliongoza taifa hili kwa miaka mitano ijayo, mojawapo ya vibali alivopata vinatokana na kazi zenu mlizozifanya ambazo zilileta mafanikio, hongereni sana” Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Gwajima

“Wapeni ushirikiano makatibu wakuu, mambo mengi yanafanywa na wataalam kwa kushirikiana na makatibu wakuu, tukikubaliana kufanya jambo basi wote tufunge mikanda kuhakikisha tukamalisha kwa wakati lengo likiwa kutimiza dhamira ya Mhe. Rais ya kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za afya nchini” Dkt. Gwajima.

“Nawataka Viongozi wa Wizara mnapoenda ‘Supervision’ mrudi na ripoti na pia nawaomba Makatibu Wakuu msizipuuze ripoti mnazoletewa ili tuone zinaleta faida gani kwenye ofisi zetu na pia katika kuboresha huduma za afya nchini” Dkt. Gwajima.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top