} });
 

 

MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Uruguay, Luis Suarez, amewaponza wafanyakazi wanne wa chuo kikuu cha Perugia nchini Italia, ambao wanashukiwa kuhusika katika udanganyifu wa Suarez kufaulu mtihani wa lugha ya Kiitaliano na kupata B1 wakati hajui lugha hiyo.

 

Suarez baada ya mambo kuwa magumu FC Barcelona alikuwa anataka kuhamia Juventus ya Italia lakini klabu hiyo walikuwa wameshamaliza nafasi za kusajili wachezaji wanaotoka nje za nchi za jumuiya ya Umoja wa Ulaya.

 

Suarez ndipo akalazimika kuomba uraia wa Italia na kutakiwa kufanya mtihani lakini inaonekana kama alidanganya kwani hajui hata kidogo Kiitaliano na inasemekana alikuwa nao mtihani siku moja kabla licha ya kufaulu mpango wake ukakwama na kuhamia Atletico Madrid.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top