} });
 

 

Huko nchini Kenya katika eneo la Baricho, Kirinyaga imetokea vuta nikuvute baada ya wasichana kudai fedha zao kwa mchungaji waliyemlipa ili awaombee wapate wanaume wa wakuwaoa.

Wasichana hao wamelalamika kuwa, maombi ya mchungaji huyo anayejiita Nabii hayajafanyakazi licha ya kulipwa fedha kwani hata salamu kutoka kwa wanaume zimekata tofauti na awali kabla hawajaombewa.

Inadaiwa kuwa Nabii huyo ambaye ni Mwanamke awali alitambulika na wengi kutokana na maombi yake kwa warembo waliokuwa hawajafanikiwa kupata waume.

Kwa mujibu wa gazeti la Taifa Leo, wasichana wengi walikuwa wakifurika kwa mama huyo kusaka maombi ambayo walilazimika kuyalipia kabla ya kuhudumiwa.

Lakini awamu hii mambo yamekuwa kinyume kwani baada ya kufanyiwa maombi inasemekana wasichana hao waliahidiwa kusubiri kwa muda wa siku tatu kabla ya kuanza kuona matokeo.

Hata hivyo siku tatu zilipita, wiki nayo pia ikaisha bila warembo kuona mabadiliko yoyote na walipogundua walikuwa wamehadaiwa waliamua kurejea kwa mama huyo.

“Tunataka hela zetu. Ulituambia tutaanza na kupata wanaume wa kutuoa baada ya siku tatu. Wako wapi.

“Juzi nilitongozwa. Hata saa mbili hazikupita jamaa akaniblock. Maombi yako ni ya laana ama Baraka,” mrembo mmoja aliwaka huku Nabii huyo akibaki mdomo wazi.

Hata hivyo baada ya kelele kuzidi mama aliwaomba awafanyie maombi mengine huku akidai kwamba huenda wasichana hao hawakuweka imani ya kutosha.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top