} });
 

 

SERIKALI  ya Eswatini imesema Waziri Mkuu wa nchi hiyo, Ambrose Dlamini, amefariki dunia, wiki nne baada ya kupatikana na virusi vya corona.

 

Taarifa ya serikali imesema kuwa  Dlamini, mwenye umri wa miaka 52, alifariki dunia Jumapili mchana hospitalini nchini Afrika Kusini.

 

Hakuna sababu ya kifo iliyotajwa, lakini hivi karibuni Dlamini alitibiwa maradhi ya Covid-19 nchini Afrika Kusini. Dlamini amekuwa waziri Mkuu wa Eswatini, ambayo zamani ilikuwa ikiitwa Swaziland, tangu mwezi wa Oktoba 2018.

 

Nchi hiyo ndogo iliyopo kusini mwa Afrika ni moja ya nchi chache ambazo bado zinatawaliwa kifalme duniani. Ikiwa na idadi ya watu wapatao milioni moja tayari imerekodi visa 6,768 vya virusi vya corona na vifo 127 vilivyohusishwa na corona, kwa mujibu wa wizara ya afya.

 

Dlamini alitangaza kuwa amepatwa na virusi vya corona tarehe 16 Novemba mwaka huu. Wakati huo alisema kuwa hakuwa na dalili na alikuwa anajihisi vyema. Wiki chache baadaye, tarehe 1 Dsemba, serikali ya Eswatini ilisemaDlamini amehamishiwa katika hospitali ya Afrika Kusini kwa matibabu, kwa lengo la kuharakisha kupona kwake.

 

Lakini Jumapili serikali ilisema kuwa Dlamini amefariki “wakati alipokuwa akipokea matibabu katika hospitali ya Afrika Kusini. Serikali kwa ushirikiano na familia yak itaendelea kulifahamisha taifa kuhusu mipango kadiri inavyoendelea,” Naibu Waziri Mkuu Themba Masuku alisema katika taarifa.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top