} });
 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Ummy Mwalimu ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Tanga (CCM) akizungumza wakati wa kikao cha kwanza cha baraza la Madiwani wa Jiji la Tanga kulia ni Katibu Tawala wa wilaya ya Tanga Faidha Salim,Mkurugenzi wa Jiji hilo Daudi Mayeji na Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa

 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Ummy Mwalimu amesema atawachukulia hatua kali za kisheria wenye viwanda ambavyo vinatiririsha maji taka yenye sumu yanayochangia uchafuzi wa  mazingira.

Kauli hiyo aliitoa leo wakati akizungumza katika kikao cha kuwaapisha madiwani wa Halimashauri ya Jiji la Tanga kilichofanyika katika ukumbi wa halimashauri ya Jiji hilo alisema kuwa atahakikisha anasimamia kwa ukaribu sheria ya utunzaji wa mazingira.

Alisema kuwa hatafumbia macho iwapo itabainika kuna kiwanda hapa ambacho kinatiririsha maji taka yenye sumu kwa makusudi katika makazi ya watu au kwenye mifereji kinyume na maelekezo ya waliyopewa ya udhibiti wa maji tiririka

“Nitahakikisha nakula nao sambamba wenye viwanda ambao bado mpaka sasa wanaendelea kutuchafulia mazingira yetu licha ya maelekezo ambayo tayari serikali ilikwisha kuyatoa ya kuhakikisha wanayatibu maji hayo kabla ya kuanza kuyamwaga kwenye mitaro”alisema Waziri Ummi.

Aidha alizitaka halimashauri zote nchini kuhakikia wanahasisha wananchi kwenye maeneo yao kujenga tabia ya upandaji wa miti ili kudhibiti mabadiliko ya tabia nchini yanayotokana na kuzalisha hewa ukaa.

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobiasi Mwilapwa akitoa salamu za wilaya hiyo alisema kuwa elimu bure imesababisha uhaba wa miundombinu ya madarasa katika shule zilizoko wilayani humo.

Alisema kuwa hali imesababisha wilaya hiyo kukumbwa na uhaba wa madarasa 44 kwa ajili ya wanafunzi wanaotarajiwa kuingia kidato cha kwanza kutokana na ongezeko la kiwango cha ufaulu katika mitihani yao ya darasa la saba.

“Kwa mwaka jana matokeo ya ufaulu wa darasa la saba yameongezeka kwa asilimia 87% hivyo kupelekea uhaba wa vyumba vya madarasa kwa wananfunxzi wanokwenda kidato cha kwanza”alisema DC Mwilapwa.

Aidha Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga Abdulrahman Shiloo aliwakumbusaha madiwani kuwa wanadeni kubwa kwa wananchi wa jiji hilo la kuwaletea maendeleo na utatuzi wa kero zilizoko kwenye maeneo yao.

“Tunajukumu la kuwasaidia wananchi kusimamia maendeleo lakini ni kuwatafutia ufumbuzi wa kero zao, niwatake mwende mkawe sehemu ya majibu ya kero zao badala ya kuwa watazamaji tuu bila kuchukuwa hatua stahiki”alisema Meya Shiloo.

Nae Katibu Tawala wa Jiji la Tanga Faidha Salimu aliwataka madiwani kwenda kuwa walinzi wa amani kwenye maeneo yao kutokana na kuibuka kwa viashiria vya uvunjifu wa amani ikiwemo vitendo vya ukabaji na wizi.

“Niwaombe mwende mkawe mabalozi wa kuhamasisha ulinzi na usalama kwenye maeneo yenu kwani tayari tunataarifa za uwepo wa vikundi vya watu ambavyo vimeanza kutishia hali ya usalama kwenye maeneo yetu,hivyo kupitia nyie mtaweza kubadilisha hiyo hali”alibainisha DAS Salim.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top