} });
 


Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Dorothy Gwajima ametembelea majeruhi wawili waliopata ajali iliyohusisha gari aina ya Coaster iliyokua ikitoka Mkoani Mwanza kuelekea Itigi kugongana uso kwa uso na lori na kusababisha vifo vya watu 15 katika eneo la Mkiwa Wilayani Ikunga Mkoani Singida.

Pamoja na kuwajulia hali majeruhi hao ambao ni aliyekua Harusi Herry Mkamwa na ndugu yake Shakila Kassim ambao wamelazwa katika Hospitali ya St. Gasper iliyopo Itigi, Waziri Dorothy pia ametembelea Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida ambapo miili 14 imehifadhiwa na kushiriki ibada ya kuaga miili hiyo ambayo inatarajiwa kusafirishwa kwenda Mwanza na Mbeya.

Waziri Dorothy pia amewafariji wafiwa na kusema kuwa Serikali iko bega kwa bega katika kuhakikisha marehemu wanasafirishwa na kuhifadhiwa katika nyumba zao za milele.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top