} });
 


Aliyekuwa beki wa Yanga, Kelvin Yondani baada ya kukaa nje nusu msimu aamejiunga na Polisi Tanzania kwa mkataba wa miezi sita.

 

Yondani amesajiliwa na timu hiyo akiwa mchezji huru baada ya kumaliza mkataba na klabu yake ya zamani Yanga na kushindwa kuongeza kutokana na kushindwana kimaslai.


Kwa mujibu wa chanzo cha ndani kutoka katika klabu ya Polisi Tanzania kilisema kuwa tayari wamemalizana na beki huyo mkongwe kwa mkataba wa miezi sita na wanaamini uzoefu alionao utasidia kuongeza nguvu ndani ya kikosi chao.

 

“Ni kweli tumemalizana nae na ataanza kuitumikia klabu yetu muda wowote kuanzia sasa akisaidiana na Iddy Moby na Mohamed Kassim kuhakikisha timu yetu inakuwa imara kwenye safu ya ulinzi,” kilisema chanzo hicho huku kikisisitiza kuwa usajili huo ni pendekezo la mwalimu.

 

“Walinzi waliopo hawana tatizo ni imara lakini mwalimu ameona kuna umuhimu wa kuongeza nguvu na ameangalia ubora wa Yondani ikiwa ni sambamba na uzoefu wake anaamini atawasaidia wachezaji waliopo,” alisema.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top