TPDC imezindua eneo la mradi wa kujenga maghala ya kuhifadhia Mafuta na gesi katika eneo la Zuzu mkoani Dodoma.
Uzinduzi huo umefanyika Juni 12, 2020 baada ya kukamilisha ulipaji wa fidia kwa wananchi 19 ambao wamelipwa zaidi ya shilingi milioni 128 kwa ajiri ya kupisha ujenzi wa mradi wa kujenga maghala ya kuhifadhia Mafuta na gesi katika eneo la Zuzu uliyozinduliwa na Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Patrobasi Katambi.
Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC Dkt.James Mataragio amesema kuwa shughuli za TPDC ni utafutaji , usambazaji na uuzaji wa Nishati ambayo ni gesi asilia na Mafuta.
“Kazi yetu kubwa ni kuhakikisha nishati inawafikia wananchi wote ili kuunga juhudi za Rais Dkt. John Pombe Magufuli za kufikia malengo ya Tanzania ya viwanda”, ameeleza Dkt. Mataragio .
Aidha Dkt. Mataragio amesema kuwa kufikia uchumi wa viwanda lazima kusambaza nishati ya uhakika ili kuleta matokeo chanya kwa wanachi kufikia adhima ya uchumi wa viwanda.
Kwa Upande wake Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Patrobas Katambi amesema kuwa ujio wa mradi wa kujenga maghala ya kuhifadhi Mafuta na gesi utafungua wigo mpana kwa wakazi wa eneo hilo katika kuleta maendeleo .
“Napenda kuwa pongeza wanachi wote wa eneo hili kwa uzalendo wenu wa kutaka kupata maendeleo kwa kupisha mradi huu katika eneo hili kwa kutaka mradi huu kutekelezwa kikamilifu ili kuleta maendeleo”, amesema Katambi.
Katambi ameongeza kuwa kitendo cha kupisha mradi huu kutekelezwa katika eneo hilo wakazi wa hapo watapata ajira,wamelipwa fidia, barabara zitajengwa na mzunguko wa pesa utaongezeka katika eneo hili hivyo wakazi wahapo wametakiwa kuutunza mradi huo ili kupata matokeo chanya kupitia mradi huo.
Naye Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira Mhe. Anthony Mavunde amewataka Wakazi wa eneo hilo kutumia fedha za fidia walizolipwa na Shirika la Maendeleo ya Petro Tanzania kuboresha maisha yao kwa kujenga vitega uchumi vitakavyowasaidia kuwaletea maendeleo.
Meneja Mkuu wa Tan Oil, Mhandisi Kapuulya Musomba amesema kuwa baada ya zoezi la kupata ardhi kukamilika sasa hataua inayofata ni kurasimisha eneo hilo liweze kupatiwa hati alafu upembuzi ya kinifu utafanyika kwa ajiri ya kuanza kutekeleza mradi huo.
Kwa upande wake
Bw.Juma Boniphace mmoja wa wakazi wa Kata ya Zuzu ambaye amepisha ujenzi huo akitoa neno la shukrani kwa niaba ya wenzake amesema kuwa wao kama wakazi wa Zuzu wanashukuru sana kwa wahusika na serikali kwa ujumla kuwaletea maendeleo na baada ya mradi huo kukamilika zuzu itabadilika sana kimaendeleo na wao wako tayari kuendeleza maendeleo hayo yatokanayo na mradi huo.