Hadi kufika jana julai 15, ikiwa ni
siku ya pili ya kuchukua na kurejesha fomu za kugombea ubunge na udiwani kwa
wanachama wa chama cha mapinduzi kote nchini, waliochukua fomu za kugombea
ubunge mkoani Kagera ni 125 ambapo jimbo la Biharamulo wafikia 40 na 7 kati ya
hao ni wanawake.
Adia Rashid Mamu katibu waCCM wilaya
ya Biharamulo alipokuwa akiongea na vyombo vya habari ofisini kwake kwa lengo
la kueleza mwenendo mzima wa uchuaji fomu unavyoenedelea wilayani humo ameeleza
kuwa wananchama katika wilaya hiyo wamehamasika na kujitokeza kutekeleza haki
yao ya kikatiba
Na kuongeza kuwa hamasa hiyo
inatokana na mambo makubwa yaliyofanywa na serikali ambayo ipo chini ya chama
chao ikiongozwa na Rais Magufuli.
Amesema kuwa uchukuaji wa fomu za
ubunge umegusa rika zote huku akionyesha kufurahishwa na wingi wa wananwake
waliojitokeza kugombea jimbo hilo pamoja na vijana na kuwataka watia nia hao
kufuata kanuni na taratibu za chama na kuongeza kuwa licha ya idadi hiyo kuwa
kubwa mbunge aliyemaliza muda wake bado hajajitokeza kuchukua fomu.
“Mwenendo wa uchukuaji fomu za ugombea hapa kwetu
unakwenda vizuri na wanachama wamehamasika kwa wingi kuchukua fomu,
kinachonifurahisha Zaidi ni kuona wanawake na vijana wamejitokeza hili
linaashiria kuwa ndani ya chama chetu demokrasia imetawala na kuonyesha uongozi
sio wa watu Fulani ” Amesema Adia
Aidha katibu huyo amesema kuwa
maandalizi kuelekea kwenye kura za maoni yapo vizuri ambapo amebainisha kuwa
katika wilaya hiyo wapo Zaidi ya wajumbe 600 ambao wote wanatarajia kushiriki
kikamilifu uchaguzi huo ndani ya Chama na hatimaye wakampata mgombea
atakayepeperusha bendera ya CCM katika uchaguzi mkuu utakaofanyika mwezi oktoba
mwaka huu.
Nje ya ofisi hiyo walikuwepo baadhi
ya watia nia ambao walikuwa wananendelea kuchukua fomu na wengine wakirudisha
fomu ambao miongoni mwa wagombea hao ni Mhandisi Ezra Chiwelesa ambaye amefika
ofisini hapo kurejesha fomu na kuwaeleza waandishi wa habari kuwa yeye kama
kijana ameamua kugombea ubunge ili kuwatumikia wanabiharamulo.
“Nimeamua kuchukua fomu ya kuomba kugombea nafasi
ya ubunge kupitia chama change nikiamini mimi na weza kuwatumikia
wananbiharamulo, chama chetu sasa ni kipya na mimi nataka Biharamulo yetu iwe
mpya na iwe sehemu ya kuwavutia wawekezaji maana tayari tunayo mbuga inayopita
kwenye wilaya yetu ya BURIGI CHATO hii ni fursa kwa wananchi wa Biharamulo.” Amesema Mhandisi Ezra.
Mwingine aliyekuwepo ni Idrissa
Songoro ambaye naye amejitokeza kuchukua fomu ya kuwania kuteuliwa kugombea
ubunge wa jimbo hilo ambapo ameeleza kuwa kutokana na demoklasia iliyopo ndani
ya chama anajiona anatosha kuwatumikia wananbiharamulo.
Katika wilaya ya Missenyi
waliojitokeza kuchukua fomu za kugombea nafasi ya ubunge wa jimbo la Nkenge
wafikia 46 hadi julai 15 mwaka huu ambapo miongoni mwa watia nia hao wamo
waliowahi kuwa wabunge wa jimbo hilo ambao ni Balozi Dkt. Deodorus Kmara mbunge
aliyemaliza Muda wake, Mhe.Asumputa Mshama aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Kibaha
mkoani Pwani.
Kwa mujibu wa Katibu wa chama hicho
wa wilaya Missenyi Emanuel Alex ameeleza kuwa miongoni mwa watia nia hao wane
kati ya hao ni wananwake huku akizidi kuhamasish wananchama kwenda kuchukua
fomu ili waweze kukipigania chama chao.
Aidha kwa upande wa Jimbo la Ngara
watia nia waliochukua fomu ya kuwania kuteuliwa kugombea ubunge wa jimbo hilo
kupitia CCM wafikia 39 hadi julai 15 mwaka huu huku mmoja kati ya hao ni
mwanamke.
Kwamujibu wa katibu wa ccm wilaya ya
Ngara Mapanga Nelele amesema kuwa mwenendo wa uchukuaji fomu unakwenda vizuri
ambapo ameeleza kuwa miongoni mwa watia nia hao yumo mbunge aliye maliza muda
wake Mhe. Alex Gashaza ambaye nay eye amechukua fomu kwaajili ya kuitetea
nafasi yake ambapo ameongeza kuwa waliochukua fomu kuwania udiwani viti maalumu
wamefikia 16.
Nelele amewasihi wagombea kuendelea
kufata kanuni na taratibu za chama katika mchakato mzima ili waweze kuenzi
katiba ya chama chao na kuwasihi wanachama kuendelea kuzitumia siku zilizobakia
kujitokeza kuchukua fomu.