} });
 

 

Kijana mmoja aliyefahamika kwa jina la Masoud Habibu Mrisho mkazi wa Kata ya Goweko wilayani Uyui mkoani Tabora amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Wilaya ya Tabora Mjini akituhumiwa kumbaka mama yake mzazi, tukio ambalo anadaiwa kulitenda majira ya usiku wakati alipokwenda Tabora mjini kumsalimia mama yake huyo.

Masoud Mrisho mwenye umri wa miaka 19 katika shauri hilo la jinai namba 1 la mwaka 2021 anadaiwa kutenda kosa hilo mnamo Desemba 16, 2020 saa tatu usiku, huko katika eneo la Kirimbika, Kata ya Isevya, Manispaa ya Tabora.

Katika maelezo ya awali yaliyowasilishwa mahakamani hapo na upande wa Jamhuri kupitia wakili wake Tumain Pius, mtuhumiwa Masoud Mrisho anadaiwa kutenda kosa hilo kinyume na Kifungu cha 138 ambapo akiwa nyumbani kwa mama yake mzazi, ilipofika usiku alimkamata kwa nguvu kisha kufanya kosa hilo la shambulio la kingono.

Mbele ya Hakimu katika mahakama hiyo ya Wilaya, John Mdoe, mtuhumiwa alikana kutenda kosa hilo na shauri hilo limeahirishwa hadi Januari 27, mwaka huu kesi hiyo itakapotajwa tena.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top