} });
 


Ajali mbaya imetokea majira ya saa 11 alfajiri ya leo Jumamosi, Januari 16, 2021, baada ya basi la abiria mali ya Kampuni ya Saratoga lilikouwa likitokea Kigoma kwenda Dar es Salaam kugongana uso kwa uso na gari ndogo ya abiria (Hiace) maeneo ya Mbezi jijini Dar.

 

Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, hakuna kifo kilichotokea ispokuwa kuna majeruhi ambao ni pamoja na kondakta wa basi hilo ambaye amevunjika mguu.

Aidha, Hiace hiyo imeharibika nyang’anyang’a huku dereva wake akisalimika na kukimbia eneo la tukio kwenda kusikojulikana. Kwa taarifa zaidi endelea kufuatia taarifa zetu.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top