} });
 

 

JESCA SAMSON  (37) mkazi wa mtaa wa Katoma, Kayanga wilayani Karagwe mkoani Bukoba, anadaiwa kujiua kwa kunywa sumu ya panya baada ya kusikia mume wake aliyefungwa kutokana na ugomvi wao ameachiwa kutoka jela. 

Mwanamke huyo, kabla ya kifo chake anadaiwa pia alimnywesha sumu hiyo mtoto wake, Jordan Samson (3), ambaye hata hivyo alinusurika kifo. 

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kagera, Revocatus Malimi, alisema tukio hilo lilitokea Januari Mosi saa 8:00 usiku baada ya mama huyo kutoka katika mkesha wa Mwaka Mpya. 

Jesca, akiwa na ndugu zake, wakitoka kwenye mkesha, alipata taarifa kuwa mume wake ameachiwa huru na baada ya kusikia hivyo, aliwaacha njiani aliokuwa nao na kuwahi nyumbani kisha akanywa sumu hiyo.

 Malimi alisema baada ya ndugu zake kufika nyumbani, Jesca aliwaambia kuwa amekunywa sumu ya panya, ndipo walimpeleka hospitali ya Wilaya Nyakahanga  na mtoto wake, ambapo mwanamke huyo alifariki dunia Januari 2, huku mtoto wake akipona.


Mumewe ambaye hakutajwa jina, alikuwa amefungwa kifungo cha miezi mitatu jela kutokana na mgogoro wa kifamilia.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top