} });
 


MSANII wa muziki Bongo, Alikiba amesema suala la uvaaji kwenye video zake halimsumbui tena maana mambo mengi ameshayapitia kwenye muziki wake na kusema kuwa kwa sasa anaangalia ubunifu mwingine.

  

”Mambo ya kuvaa sijui hereni masikioni na vitu vingine vya aina hiyo, nadhani kwangu muda wake ulishapita.Hata mitindo yangu ya sasa kuanzia uvaaji wangu kwenye video nadhani unafaa kwasababu watu wanaohusika na ubunifu wanafanya kazi yao,” amesema Alikiba.

  

Katika hatua nyingine Alikiba amesema moja ya sababu kubwa ya kuimba kwa lugha ya kifaransa kwenye ngoma yake mpya Infidele ni kutokana na lugha hiyo kutumiwa na watu wengine duniani hivyo kuna uwezekano wa muziki wake kuwafikia watu wengi.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top