} });
 


Saidi Kihundwa (98), Mkazi wa Kijiji cha Mlangoni katika Kata ya Gararagua, Wilaya ya Siha mkoani Kilimanjaro, anadaiwa kuuawa kikatili na mjukuu wake, aliyeona babu yake anateseka na maradhi kwa muda mrefu.


Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani Kilimanjaro, Kamishna Msaidizi Leonard Makona, alithibitisha taarifa za kuuawa kwa mkazi huyo.


Tukio hilo lilitokea wiki iliyopita, majira ya jioni nyumbani kwa mzee huyo, mjukuu wake akidaiwa kumpiga na kitu kizito kichwani na kumsababishia umauti.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top