} });
 

 

MWANAMME mwenye umri wa miaka 56 ambaye hakutambuliwa zaidi amekamatwa na mamlaka nchini Austria katika uwanja wa ndege wa Vienna akiwa anatorosha vinyonga 74 kutoka nchini Tanzania.

 

Kwa mujibu wa gazeti la The Telegraph la Uingereza jamaa huyo alikuwa amewaficha wanyama hao katika soksi na masanduku ya barafu alipokamatwa na maofisa forodha wa uwanja huo wa Vienna.

 

 

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii nchini Tanzania, Allan Kijazi, amesema mwanamme huyo alisafiri kwenda Austria kutoka Tanzania kupitia Ethiopia na kwa  mujibu wa gazeti hilo vinyonga hao walikuwa wakipelekwa kwenye bustani ya wanyama ya Schoenbrunn na ilibainika kuwa watatu wamekufa.

 

Amesema wanyama wote walikuwa wanatoka katika milima ya Usambara Tanzania na walikuwa katika umri wa wiki moja hadi wakubwa ambao walitakiwa kuuzwa katika masoko ya ulanguzi.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top