} });
 


DESEMBA 11, 2020, Mastin Mukanga alifunga pingu za maisha na Linet Kavere katika harusi maridadi lakini bibi harusi aliaga dunia siku 18 baadaye.

 

Wawili hao walikutana katika Chuo Kikuu cha Masinde Muliro wakiwa wanafunzi na kuanza kuwa marafiki wa dhati na kisha baadaye kuchumbiana baada ya kumaliza chuo.

 

Mastin alipata ajira kama Mhandisi katika Shule ya Msingi ya Phanero mjini Mbale huku Linet akipata nafasi ya ualimu katika Shule ya Wasichana ya Mbihi.

 

Waliidhinishwa rasmi kuwa mume na mke kwenye harusi iliyoandaliwa katika bustani ya Sosa, Desemba 2020.

 

Wakati wanandoa hao wakirejea kutoka katika fungate lao, waliazimia kuishi maisha ya raha mstarahe hadi kifo kitakapowatenganisha.

 

Lakini walitenganishwa siku moja baada ya fungate huku Linet akianza kukumbana na matatizo ya kupumua, akazirai na kisha kukimbizwa katika Hospitali ya Kisumu Specialists ambapo alithibitishwa kufariki saa chache baadaye.Humphrey Odanga, mwalimu mkuu wa shule ya Mbihi, ambapo marehemu alikuwa akihudumu, alimsifu marehemu Linet kwa kuwa mwalimu mwenye bidii.

 

“Alikuwa nasi karibu miaka miwili, pamoja na kuugua magonjwa ya kawaida kama mtu yeyote, hakuonyesha dalili zozote za kuwa na changamoto za kiafya,” alisema.

 

Kulingana na Bi. Jane Ambani, rafiki wa familia hiyo, kifo chake cha ghafla kiliwashtua wengi. “Bibi harusi  hakuwa hata hajaanza kuishi kwenye nyumba ya mumewe tangu harusi yao,” alisema.

 

Linet alizikwa Jumamosi, Januari 9, 2021 Matokeo ya upasuaji yalionyesha kuwa Linet alikumbwa na shinikizo la damu.


Wafanyakazi wenzake  na marafiki zake walitoa rambi rambi zao kufuatia kifo chake.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top