} });
 

 

MWANDISHI wa habari nchini Hispania, Jose Ramon de la Morena amefichua kuwa ni bora Diego Costa ameamua kuondoka ndani ya Atletico Madrid, hiyo ni kwa kuwa ilibaki kidogo achapane makonde na msaidizi wa kocha wake mkuu.


Inaelezwa kuwa mara baada ya kutokea kwa mzozo huo wa Costa na Nelson Vivas, ilibidi kocha mkuu Diego Simeone aingilie kati na kuamua ugomvi wao.


Taarifa zinaeleza kuwa kuanzia mwanzoni mwa msimu huu, Costa alikuwa njiani kuondoka kutokana na matatizo yake ya kifamilia, lakini kulikuwa na ugumu wa kuruhusiwa kuondoka.

 

Wakati mzozo wa mkataba wake ukiendelea, ndipo kuna siku alipishana kauli na msaidizi huyo na kilichotokea ilikuwa ni ugomvi mkubwa baina yao, lakini mwisho Costa alivunja mkataba na sasa ni mchezaji huru

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top