} });
 


Jeshi la Polisi mkoa wa Tanga, linamshikilia Simon Pasian Tarimo, mwenye umri wa miaka 37, dereva na mkazi wa Kimara jijini DSM, akisafirisha mirungi bunda 1,685 sawa na kilogramu 133, akiwa ameweka kwenye jokofu linalotumika kuhifadhia jeneza lenye maiti wakati wa kusafirisha.

Taarifa hiyo imetolewa na Kamanda wa Polisi mkoa wa Tanga, Blasius Chatanda, na kusema kuwa mtuhumiwa huyo alikamatwa majira ya saa 2:00 usiku huko katika Kijiji cha Manga, Kata ya Mkata, Tarafa ya Mazingara wilayani Handeni mkoani Tanga, ambapo mirungi hiyo ilikuwa ikisafirishwa kutoka Usangi kupelekwa Dar es Salaam, ikiwa imehifadhiwa kwenye gari maalumu la kubebea maiti.

“Mbinu iliyotumika ni kuweka mifuko kwenye jokofu linalotumika kuhifadhia jeneza lenye maiti wakati wa kusafirisha, kitendo ambacho ni kinyume cha matumizi ya gari hilo”, Kamanda Chatanda. 

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top