} });
 


RAIS wa Marekani Donald Trump amesema kwamba hotuba yake ya wiki iliopita alipowataka wafuasi wake kuvamia bunge la Congress ‘ilistahili’.


Bwana Trump alisema kwamba ni upuuzi kwa wanachama wa Democrarts kuweka juhudi za kumshataki bungeni kwa ‘kuchochea uasi’.


Anaondoka afisini tarehe 20 Januari wakati ambapo rais mteule Joe Biden ataapishwa.


Bunge la uwakilishi linatarajiwa kupigia kura kifungu cha sheria kuhusu kumshtaki rais huyo siku ya Jumtano.

 

”Nadhani mchakato huo wa kunishtaki unasababisha hatari kubwa kwa taifa letu na unasababisha hasira kubwa . Sitaki ghasia” , bwana Trump alisema.


Alikuwa akizungumza alipokuwa akiondoka katika Ikulu ya Whitehouse kuelekea jimbo la Texas ili kuchunguza sehemu moja ya Ukuta uliojengwa katika mpaka wa taifa hilo na Mexico.


Ilikuwa mara ya kwanza kwa yeye kuonekana hadharani tangu ghasia za Capitol ambapo takriban watu watano walifariki na makumi kujeruhiwa ikiwemo maafisa wa polisi 60.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top