} });
 

 

Tajiri namba moja nchini China, Jack Ma.

Ukiona mtu amefanikiwa maishani, usidhani ni kazi rahisi! Nyuma ya mafanikio ya watu wengi unaowajua hii leo, kuna maumivu, msoto, kudharaulika na kila aina ya taabu.

 

Hivyo ndivyo ilivyotokea katika maisha ya bilionea mkubwa duniani kwa sasa na mmiliki wa mtandao maarufu wa kuuza bidhaa mtandaoni wa Alibaba! Namzungumzia Jack Ma, bilionea mkubwa kuliko wote nchini China na miongoni mwa watu wachache wanaoongoza kwa kuwa na utajiri mkubwa duniani.

 

Kama ulikuwa hujui, ripoti mpya ya Forbes, inaonesha kwamba mpaka Januari 5, 2021, utajiri wa Jack Ma ni dola bilioni 57.9, akishika nafasi ya 17 katika orodha ya mabilionea duniani lakini pia akishika nafasi ya kwanza kwa utajiri nchini China.


Unaweza kudhani safari ya bilionea huyu ilikuwa nyepesi, la hasha! Historia ya maisha ya Jack Ma imejawa na misukosuko mingi sana, kama angekuwa mtu wa kukata tamaa, pengine leo hii dunia isingekuwa inamtambua.

 

Unataka kumjua Jack Ma na historia ya maisha yake? Twende pamoja kuitazama safari yake ilivyokuwa, tangu anazaliwa mpaka sasa.


JACK MA NI NANI?

Jack Ma alizaliwa Septemba 10, 1964 katika mji wa Hangzhou, Zhejiang nchini China katika familia ya kifukara kabisa. Alizaliwa katika familia ya watoto watatu na kutokana na umaskini wa wazazi wake, maisha yake ya utotoni yalijawa na msoto wa nguvu.

 

Tangu akiwa mdogo, Jack Ma alionesha kuvutiwa sana na lugha ya Kiingereza, akaanza kujifunza kwa bidii. Kwa kuwa wazazi wake hawakuwa na uwezo wa kumpeleka kwenye shule nzuri ambayo ingemfanya akijue vizuri Kiingereza, aliamua kujiongeza.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top