} });
 

 

NYOTA wa muziki wa Hip Hop nchini Uganda, Joseph Mayanja maarufu kama Jose Chameleone, ni miongoni mwa wagombea wa nafasi ya meya wa jiji la Kampala.

 

Uchaguzi wa viongozi wa serikali za mitaa unafanyika leo nchini Uganda, pamoja na Meya wa majiji kukiwa na ushindani mkali katika jiji la Kampala.

 

Meya anayetetea kiti chake ni Elias Lukwango wa chama cha FDC  ambaye anakabiliwa na ushindani mkali kutoka kwa msanii Jose Chameleon ambaye ni mgombea wa kujitegemea, na msanii mwingine anayewania kiti hicho ni Daniel Kazibwe maarufu kama Ragga D kutoka chama tawala na mgombea mwingine ni Nabilah Naggayi kutoka chama cha Bobi Wine.

 

Wakati huohuo tume ya uchaguzi  imepokea matokeo ya vituo 1,200 vya kupiga kura ambavyo havikujumuishwa wakati akitangazwa rais Museveni kuwa mshindi.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top