} });
 

 

Rais Dkt.John Magufuli amemuagiza Waziri wa Afya Dkt. Dorothy Gwajima, kumfuatilia daktari aliyeacha kazi katika hospitali ya rufaa mkoa wa Tabora kwa sababu ya maslahi madogo na kuhamia hospitali binafsi na ikiwezekana afungiwe yeye pamoja na hospitali aliyoikimbilia.

Rais Magufuli ametoa kauli hiyo wakati akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa jengo la magonjwa ya dharura Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tabora amabapo amesisitiza kuwa "Madaktari wanapata mkopo 100%  wakiwa Chuoni, halafu tunawapa ajira Serikalini wanakimbia kisa maslahi, si ungekimbia wakati unasoma?, hela yetu umekula halafu unakimbia kwenda Hospitali binafsi kwa kisingizio cha maslahi, ni kukosa uzalendo"

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top