} });
 

 

MAJINA mawili yamepitishwa katika kumpata kocha mkuu na kocha wa makipa ndani ya kikosi cha Simba ambacho kwa sasa kinasaka warithi wake.

 

Hiyo ni baada ya Bodi ya Wakurugenzi ya Klabu ya Simba kutangaza nafasi ya kazi ya ukocha atakayekuja kumrithi Mbelgiji, Sven Vandenbroeck.

 

Kabla ya Sven aliyekuwa kocha mkuu wa kikosi hicho kuondoka, Simba ilianza kwa kuachana na kocha wa makipa, Muharami Mohamed.

 

Viongozi hao wa bodi tayari wamepokea CV mbalimbali za makocha wa kigeni walioomba kibarua cha kukinoa kikosi hicho kilichofuzu hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

 

Spoti Xtra, limejiridhisha kuwa Simba tayari imempata kocha mkuu na kocha wa makipa ambao wote hadi kufikia kesho Ijumaa watakuwa wametua nchini tayari kujiunga na kambi ya timu hiyo.

 

Bosi mkubwa ndani ya Simba alisema makocha hao wote mara baada ya kutua nchini moja kwa moja wataingia kambini tayari kwa ajili ya kuanza kibarua cha kukinoa kikosi hicho.

 

“Tayari tumewapata makocha wawili ambao wote haraka watajiunga na timu Ijumaa mara baada kuwasili nchini tayari kwa kuanza kazi.“

 

Kati ya makocha hao, mmoja mkuu na mwingine wa makipa ambao wamepitishwa na kikao cha Bodi ya Wakurugenzi wa Simba waliokutana juzi,” alisema mtoa taarifa huyo.Mtendaji Mkuu wa Simba, Barbara Gonzalez, juzi alisema: “Makocha wengi wameomba kazi ya kuiongoza Simba.”

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top