} });
 


Mbunge mpya mwanamke aahidi kutembea na bunduki wakati wa muhula wake huko Washington DC, Lauren Boebert ambaye ni Mbunge kupitia Chama cha Republican toka Washington DC, hata wakati wa kampeni zake alikuwa anasisitiza suala la kumiliki na kutembea na bunduki.

Mbunge huyo amesema, yeye kama mwanamke anaweza kujilinda mwenyewe hivyo atajilinda mwenyewe kwa kushika bunduki.

Aidha, Mkuu wa Polisi wa Washington DC, Robert Contee III amesema, “Mbunge atakabiliwa na adhabu ile ile kama mtu mwingine yeyote anayepatikana akiwa amebeba silaha katika Mji wa Washington DC”.

Sheria za Umiliki wa Bunduki nchini Marekani ziko tofauti kutokana na Majimbo na Wabunge wanaruhusiwa kumiliki bunduki katika ofisi zao na kusafiri nazo mjini Washindton DC mradi zisiwe na risasi.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top