} });
 

 

MGOMBEA useneta wa chama cha Democratic nchini Marekani, Mchungaji Raphael Warnock, ameshinda katika kura za marudio dhidi ya mgombea wa chama cha Republican, Kelly Loeffler, shirika la habari la NBC la nchini humo limesema.


Vilevile, mgombea wa Democrat, Jon Ossoff, alimshinda yule wa Republican, David Perdue, hivyo kumfanya Rais Mteule, Joe Biden kuwa na Baraza la Seneti lenye wabunge wengi kutoka chama cha Democrat.

 

“Tuliambiwa tungeshinda katika uchaguzi huu, lakini leo tumethibitisha kwamba matumaini, kazi kubwa na watu wakiwa upande wetu,  chochote kinawezekana,” alisema  Warnock kwa wafuasi wake.Alisema anatumaini ushindi wake utawachochea vijana wenye ndoto zao kuhusu Marekani.


“Georgia imenipa heshima,” alisema Warnock na kuongeza: “Ninakwenda katika Baraza la Seneti kuwafanyia kazi watu wa Georgia.”soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top