} });
 


Mchezaji wa Kijapan mwenye umri mkubwa Kazuyoshi Miura (54) anarudi tena uwanjani baada ya kuongeza mkataba wa mwaka mmoja na club yake ya Yokohama.

Kazuyoshi Miura atatimiza umri wa miaka 54 kamili February 26 2021 ikiwa ni siku moja kabla ya kuanza kwa msimu wa 2021 wa Ligi Kuu Japana (J-League).

Huo utakuwa ni msimu wake wa 17 akiwa na club ya Yokohama toka pale alipojiunga nayo 2005.

Mara ya mwisho Miura anafunga goli ilikuwa 2017 dhidi ya Thespakusatsu Gunma katika Ligi daraja la pili na kuandika rekodi ya kuwa mchezaji mwenye umri mkubwa (miaka 50 na siku 14) kufunga goli katika professional League nchini Japan.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top