} });
 


Mtu mmoja aliyefahmika kwa jina la Ally Ismail Machulila mkazi wa Ruwelu Mikindani Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara Mkoani Mtwara amefariki dunia baada ya kusombwa na maji ya mafuriko akiwa na pikipiki yake wakati akivuka barabara eneo la Magomeni Matopeni kufuatia mvua kubwa zinazonysha Mkoani Mtwara.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Bwana Gelasius Byakanwa kwenye kikao cha Bodi ya Barabara ya Mkoa wa Mtwara.

Kufuatia hali hiyo Mkuu huyo wa Mkoa ametoa agizo kwa Wakala wa Barabara za Vijijini na Wakala wa Barabara Tanzania, kufuatilia uharibifu wa miundombinu ya barabara iliyotokana na mvua hizo. 

Hata hivyo baadhi ya familia zilizoathiriwa na mvua hizo na kupata hifadhi kwenye Gereza la Watoto, Mtaa wa Mbezi Matopeni walikuwa na maombi kwa serikali ya kujengewa mtaro kunusuru maisha yao. 

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top