} });
 

 

Ikiwa imetimia mwaka mmoja tangu kuuawa kwa Kiongozi wa Ngazi ya Juu wa Jeshi la Iran, Qasem Soleimani, Nchi hiyo imeendelea kusema italipiza kisasi dhidi ya Marekani.

Kumekuwa na mikusanyiko mikubwa ya watu iliyodumu kwa takriban wiki moja sasa katika maeneo kadhaa, kama sehemu ya kumuenzi Soleimani aliyeuawa Januari 03, 2020.

Siku chache zilizopita, Rais Hassan Rouhani alisema, kuuawa kwake ni uhalifu usioweza kusamehewa na kisasi kitaamuliwa kwa wakati sahihi.

Aidha, Jaji Mkuu wa Iran, Ebrahim Raisi amesema, Marekani ingoje kisasi cha nguvu kwa uhalifu iliyoutenda huku akionya kuwa wote waliohusika hawatakuwa salama.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top