} });
 


MWALIMU ambaye ni mke wa mtu amekutwa na hatia baada ya kukutwa na hatia ya kumshawishi mwanafunzi wake wa kiume mwenye umri wa miaka 15 kujiingiza katika masuala ya mapenzi na kufanya naye mapenzi jambo ambalo ni kinyume cha sheria.

Kandice Barber, 35, kutoka Wendover, Buckinghamshire nchini Marekani amekutwa na hatia hiyo katika Mahakama ya Aylesbury Crown na atahukumiwa jela kwa miaka mitano ambapo hukumu hiyo inatarajiwa kutolewa Februari 15, katika Mahakama ya Aylesbury Crown.

Imeelezwa kuwa, Mwezi Septemba alimshawishi mtoto huyo  kwa kumtumia picha za ngono kupitia mtandao wa Snapchat tukio alilofanya mwaka 2018, baada ya kumpiga picha mtoto huyo aliyekutana naye mazoezini, kuzitengeneza na kumtumia picha hizo akimbusu shingoni.

Mwendesha mashtaka wa Serikali, Richard Milne ameelezwa kuwa, Barber alianza kumtongoza mtoto huyo (hajatajwa jina kwa sababu za kisheria) na kuchukua simu yake kisha kuiunganisha na Snapchat, September 2018 ambapo alituma picha hiyo mtandaoni.

Wiki mbili baadaye, Barber alimshawishi mtoto huyo na kumchukua kwenye gari lake mwezi Oktoba 2018 kisha kwenda naye sehemu za faragha ambapo alitimiza adhima yake ya kufanya nae ngono.

Mwanasheria wa Barber amesema mteja wake ni mrefu sana asingeweza kufanya mapenzi na mtoto huyo wakati akiwa amesimama huku akiongeza kuwa mwalimu huyo alikuwa bize sana kiasi cha kwamba asingeweza kupata muda wa kufanya mapenzi na kijana huyo.

Mumewe na Barber aitwaye Daniel amesema kuwa tukio hilo lilikuwa ni utani na si kwamba mkewe amefanya mapenzi na mtoto huyo huku Barber mwenyewe akijitetea kuwa kijana huyo ni sawa na mtoto wake hivyo hawezi kufanya naye mapenzi.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top