} });
 


MWANAMUZIKIaliyekula chumvi nyingi kunako Bongo Flevani, Mwasiti Almasi ‘Mwasiti’, naye amefunguka juu ya wimbi la wasanii kuacha muziki akisema kwa upande wake bado hajawaza wala kufikiria kuachana na masuala ya muziki.

 

Mwasiti amesema kuwa, amekuwa akisakamwa na baadhi watu wakisema kwamba umri wake umekweda hivyo anatakiwa kuwaachia vijana kazi hiyo.

 

Mwasiti anasema kuwa, atafikia uamuziki siku ambayo Beyonce wa Marekani naye ataacha muziki.“Kwani nikiwa ninafanya muziki kuna mtu ninamkera?

 

Watu wanatakiwa kufanya mambo yao waache kufuata ya watu kwani wataangukia pabaya, mimi siwezi kuachana na kuimba labda mpaka siku Beyonce akiaacha,” alisema Mwasiti aliyedumu kwenye gemu kwa zaidi ya miaka 15 sasa.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top