} });
 

 

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mh. Khamis Hamza Chilo (Mb) akiwasili katika ofisi za Makao Makuu ya Jeshi la Polisi Nchini zilizopo Dodoma, Katika ziara hiyo amelipongeza Jeshi la Polisi nchini kwa kuendelea kutekeleza majukumu yake ipasavyo ya kudumisha Usalama wa Raia na mali zao.

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mh. Khamis Hamza Chilo (Mb) akisalimiana na Makamishna wa Jeshi la Polisi baada ya kuwasili katika ofisi za Makao Makuu ya Jeshi la Polisi Dodoma.

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mh. Khamis Hamza Chilo (Mb) akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) Simon Sirro kuhusu Jengo la Makao Makuu ya Jeshi la Polisi Nchini lililopo Dodoma ambapo ameaidi kushirikiana na Jeshi la Polisi kwa kuhakikisha Jengo hilo linakamilika kwa asilimia mia moja ili Watendaji wake waweze kutekeleza majukumu yao katika mazingira mazuri.

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mh. Khamis Hamza Chilo (Mb) akisaini kwenye kitabu cha wageni katika ofisi ya Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP) Simon Sirro Dodoma. Naibu waziri amefanya ziara ya Kikazi katika Ofisi za makao makuu ya Jeshi laPolisi kujionea namna ya utendaji kazi wa Jeshi hilo.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top