} });
 


NDOA ya mastaa wakubwa duniani, rapa Kanye West na mwanamitindo Kim Kardashian imefikia mwisho ambapo wawili hao wameripotiwa kuachana baada ya kukaa kwenye ndoa kwa miaka sita.

 

Vyanzo mbalimbali vimeiambia tovuti ya Page Six kwamba talaka tayari imetolewa na wawili hao ambao tayari mpaka sasa wana watoto wanne, wameachana rasmi.


“Wanafanya kimyakimya lakini ndiyo wameshamalizana. Kim ameajiri mwanasheria wa talaka, Laura Wasser, na wapo kwenye mazungumzo ya namna ya kumalizana,” kilisema chanzo hicho.

 

Kim Kardashian (40), hajaonekana kuvaa pete ya ndoa katika kipindi cha hivi karibuni na Kanye West (43), ameendelea kubaki mjini Wyoming katika kipindi chote cha sikukuu badala ya kuutumia muda na familia yake. Taarifa zingine zinasema walikuwa wakiishi kila mmoja kivyake miezi michache iliyopita.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top