} });
 


Klabu ya Yanga imemtangaza rasmi mchezaji wake wa zamani na kocha wa African Lyon, Nizar Khalfan kuwa kocha wao msaidizi akiziba pengo lililoachwa na kocha Juma Mwambusi aliyejiengua hivi karibuni kutokana na sababu za kiafya.

Kwa mujibu wa Afisa Habari wa timu hiyo Hassan Bumbuli, Nizar amepata nafasi hiyo baada ya kupita kwenye usaili uliofanyika Ijumaa ya Januari 22, 2021.

Bumbuli amebainisha kuwa kulikuwa na makocha takribani 10 waliojitokeza kuisaka nafasi hiyo na watano walifikia hatua ya mwisho(fainali) akiwemo Salvatory Edward, Maalim Saleh na Omary Kapilima.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top