} });
 


RAIS wa Zambia, Edgar Lungu, amemfuta kazi waziri wa afya nchini humo, Chitalu Chilufya, ambaye mwezi Juni mwaka jana alikamatwa kwa tuhuma za rushwa kabla ya kufutiwa tuhuma hizo.

 

Chilufya amekuwa akikabiliwa na mashtaka mbalimbali likiwemo larushwa ya $17m (takribani shilingi bilioni 40) iliyohusisha usambazaji wa glovu za upasuaji na mipira ya kuzuia mimba.

 

Hata hivyo Ikulu ya Zambia haijatoa maelezo ya sababu za kufutwa kazi kwa waziri huyo huku kiongozi wa upinzani nchini humo, Hakainde Hichilema, akisema hatua hiyo “imechelewa mno”.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top